Sera ya Faragha
Tarehe ya kuanza kutumika: 19/04/2025
​
Safrada Company Limited chini ya jina lake la biashara lilosajiliwa la Vitumark Shopping ("tu-", "-etu", au "sisi") imejitolea kulinda faragha yako. Sera hii ya Faragha inabainisha jinsi tunavyokusanya, kutumia, na kulinda taarifa zako za kibinafsi unapotembelea au kufanya ununuzi kutoka kwa tovuti yetu ("vitumark.com").
​
1. Maana ya Maneno
-
Tu-, -etu, au sisi: Safrada Company Limited na chini ya jina lake la biashara Vitumark Shopping.
-
Taarifa Binafsi: Taarifa kuhusu mtu anayetambulika ambazo zimeandikwa kwa njia yoyote ile, ikiwa ni pamoja na majina, anuani, barua pepe, namba za simu, taarifa za malipo, na historia ya manunuzi.
-
Mhusika wa Taarifa: Mtu ambaye taarifa zake binafsi zinakusanywa au kuchakatwa.
-
Uchakataji: Shughuli yoyote inayofanyika kwenye taarifa binafsi, ikiwa ni pamoja na ukusanyaji, uhifadhi, matumizi, ufunuaji, au ufutaji.
2. Taarifa Tunazokusanya
-
Utambulisho na Mawasiliano: Jina kamili, barua pepe, namba ya simu, na anuani ya makazi.
-
Taarifa za Malipo: Njia ya malipo na maelezo ya bili (yanayochakatwa kupitia watoa huduma wetu).
-
Maelezo ya oda: Taarifa zinazohusiana na manunuzi, usafirishaji, na utoaji wa bidhaa.
-
Taarifa za Kuingia (Login): Ikiwa utajiandikisha au kuingia kwa kutumia akaunti ya Google.
-
Taarifa za Uchambuzi: Ukusanyaji taarifa zisizo binafsi kama aina ya kivinjari, kurasa ulizotembelea, anwani ya IP, maelezo ya kifaa, na muda uliotumia kwenye tovuti yetu.
3. Matumizi ya Taarifa Zako
-
Kuchakata, kuthibitisha, na kusafirisha oda yako.
-
Kuwasiliana nawe kuhusu oda yako au maombi ya msaada kwa wateja.
-
Kufuata masharti ya kisheria, kama ya kikodi au kihasibu n.k.
-
Kukutumia jarida au matangazo kwa barua pepe ikiwa utachagua kujiunga.
-
Kukutumia uthibitisho wa oda kupitia WhatsApp (ikiwa namba yako inatumika kwenye WhatsApp).
4. Msingi wa Kisheria wa Uchakataji
-
Ridhia: Unapotoa taarifa kwa hiari au kujiunga na jarida letu.
-
Mahitaji ya Mkataba: Kutekeleza wajibu wetu wa kuchakata na kuwasilisha oda yako.
-
Wajibu wa Kisheria: Kutii sheria na kanuni husika.
5. Huduma za Washirika Wetu
-
Watoa Huduma za Malipo: Ili kufanikisha ununuaji wa bidhaa.
-
Washirika wa Usafirishaji: Kwa ajili ya kusafirisha bidhaa ulizonunua.
-
Huduma za Jukwaa: Kuhifadhi na kusimamia tovuti na taarifa zako kwa usalama.
-
Huduma za Kuingia: Unaweza kutumia akaunti yako ya Google kuingia.
Hatuuzi wala kukodisha taarifa zako binafsi kwa watu watoa huduma.
6. Vidakuzi na Uchambuzi
Tovuti yetu hutumia vidakuzi (cookies) kuboresha uzoefu wako wa kuvinjari na kuchambua trafiki kupitia Wix Analytics. Unaweza kudhibiti vidakuzi kupitia mipangilio ya kivinjari chako.
7. Uhifadhi wa Taarifa
Tunahifadhi taarifa zako binafsi kwa muda unaohitajika kutimiza madhumuni yaliyoainishwa katika sera hii, ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kisheria, kihasibu au kikodi.
8. Haki Zako
-
Kupata Taarifa: Kuomba kuona taarifa zako binafsi.
-
Marekebisho: Kuomba marekebisho ya taarifa zisizo sahihi au zisizokamilika.
-
Kufutwa: Kuomba taarifa zako binafsi zifutwe, kutegemea na masharti ya kisheria.
-
Kuzuia Uchakataji: Kuomba uchakataji usitishwe katika hali fulani.
-
Kupinga: Kupinga uchakataji unaofanywa kwa misingi ya maslahi halali.
Ili kutumia haki zako, wasiliana nasi kupitia: vitumarkshopping (at) gmail. com
9. Kizuizi cha Umri
Tovuti yetu imelenga watu walio na umri wa miaka 18 na zaidi. Hatukusanyi taarifa kutoka kwa watoto wadogo kwa makusudi.
10. Usalama wa Taarifa
Tunategemea miundombinu salama ya Wix kuhifadhi na kusimamia taarifa. Ingawa hakuna mfumo ulio salama kwa asilimia 100, tunachukua hatua stahiki kulinda taarifa zako binafsi.
11. Uhamishaji wa Taarifa Kimataifa
Iwapo tutahamisha taarifa zako binafsi nje ya Tanzania, tutahakikisha kuwa nchi husika ina sheria za kulinda taarifa, kulingana na makubaliano yako na sisi katika sheria na masharti yetu.
12. Mabadiliko ya Sera Hii
Tunaweza kusasisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara kuonyesha mabadiliko ya utendaji wetu au masharti ya kisheria. Mabadiliko yatawekwa katika ukurasa huu na tarehe mpya ya kuanza kutumika.
​
13. Wasiliana Nasi
Kwa maswali kuhusu Sera hii ya Faragha au taarifa zako binafsi, wasiliana nasi kupitia:​
-
📧 vitumarkshopping (at) gmail. com
-
📞 +255 715 842 928
​
​