Vigezo & Masharti
Tarehe ya Kuanza Kutumika: 23/04/2025
Masharti haya yanaelezea sheria za matumizi ya tovuti ya "vitumark.com". ya Safrada Company Limited, inayofanya biashara kwa jina la Vitumark Shopping ("tu-", "-etu", “sisi”). Huduma na bidhaa za vitumark.com zinauzwa na kutolewa na, na unaingia katika mkataba na: Safrada Company Limited.
Vitumark shopping
Safrada Company Limited
P. O. Box 275
Tanga, Tanzania
Brela Reg. No. 182936286
Business Licence No. BL01860002024-2500004594
Kwa kutumia tovuti hii, unakubaliana na masharti haya.
​
1. Sifa na Masharti ya Umri
Tovuti hii inakusudiwa kwa watumiaji walio na umri wa miaka 18 na kuendelea. Hatukusanyi kwa makusudi taarifa binafsi kutoka kwa watu walio chini ya umri huo. Wazazi na walezi wanapaswa kusimamia matumizi ya intaneti ya watoto wao. Iwapo wewe ni mzazi au mlezi unayejulikana kisheria na unamruhusu mtoto wako atumie tovuti hii, basi sheria na masharti haya yanatumika kwako na unawajibikia shughuli za mtoto wako kwenye tovuti hii.
​
2. Usajili wa Akaunti
Usajili wa akaunti ni hiari. Manunuzi yanaweza kukamilika bila kusajili akaunti. Akaunti zinaweza kusaidia katika huduma za baadaye kama ufuatiliaji wa historia ya oda zako.
​
3. Matumizi Yasiyoruhusiwa
Watumiaji hawaruhusiwi:
-
Kuchapisha tena, kunakili, kusambaza au kutumia tena maudhui yoyote kutoka Vitumark.
-
Kutumia utambulisho wa Vitumark Shopping au wafanyakazi wake bila ridhaa.
-
Kutumia tovuti kwa madhumuni yoyote haramu, yenye madhara, ya ulaghai au hasidi.
-
Kutuma matangazo taka, kudukua au kukwepa mifumo au hatua zetu za ulinzi.
-
Kushiriki katika matumizi mabaya au shughuli yoyote ambayo inatatiza utendakazi wa Tovuti.
​
4. Bidhaa na Upatikanaji
Vitumark huuza vifaa vya kielektroniki, na bidhaa nyingine kama vifaa vya nyumbani, teknolojia, bidhaa za usafiri, n.k.
Tunaweza kuuza bidhaa mpya, zilizotumika, na zilizorekebishwa. Bidhaa zote zitauzwa zikiwa katika hali nzuri na salama kutumia isipokuwa tu kama itaelezwa vinginevyo.
Bei na upatikanaji wa bidhaa vinaweza kubadilika bila taarifa.
​
5. Matengenezo, Marejesho na Dhamana
Vitumark haitoi marejesho au ubadilishaji wa bidhaa. Bidhaa chache zinaweza kupata huduma ya matengenezo, bila kujumuisha gharama za vipuri na usafiri, pale tu inapobainishwa kwenye maelezo ya bidhaa. Matengenezo sio sehemu ya makubaliano ya manunuzi ni ofa itakayoambatanishwa na baadhi ya bidhaa.
​
6. Malipo na Uwasilishaji
Tunapokea njia zifuatazo za malipo:
-
Kadi za Visa na Mastercard
-
Huduma za pesa za simu zinazopatikana Tanzania
Muda wa kutuma mzigo: Siku 3.
Njia za Kusafirisha: Mabasi ya mikoani au huduma za usafirishaji wa mizigo/parcel, kulingana na eneo na gharama. Hatutoi nambari za ufuatiliaji (tracking number).
​
7. Usindikaji wa Data na Uhamisho wa Kimataifa
Kwa kutumia tovuti hii na kutoa taarifa zako, unatoa idhini yako ya kukusanywa, kuchakatwa, na kuhifadhiwa kwa taarifa zako, ikiwemo kuhamishwa kwa data nje ya Tanzania, kwani baadhi ya watoa huduma wetu wapo nje ya nchi.
Tunachukua hatua stahiki kuhakikisha data zako zinalindwa kwa mujibu wa sheria za ulinzi wa data Tanzania.
8. Ukomo wa Uwajibikaji
Vitumark haitawajibika kwa:
-
Muda wa ucheleweshaji wa usafirishaji unaosababishwa na wahusika wengine.
-
Makosa ya malipo yanayofanywa na mteja au mfumo wa malipo ya simu.
-
Madhara yoyote yatokanayo na taarifa za uongo zilizotolewa na mteja.
-
Taarifa ambazo si sahihi, zimepitwa na wakati, au hazijakamilika kwenye tovuti.
-
Tovuti kutopatikana au matatizo ya kiteknolojia.
9. Haki Miliki
Maudhui yote ya tovuti, ikiwa ni pamoja na maandishi, picha, alama, na maelezo ya bidhaa, ni mali ya Vitumark au watoa leseni wake. Haifai kutumia au kusambaza tena bila ruhusa.
​
10. Uzingatiaji wa Sheria
Tovuti hii inafanya kazi chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
​
11. Mabadiliko ya Masharti
Vitumark ina haki ya kubadili masharti haya wakati wowote. Toleo jipya litawekwa kwenye ukurasa huu pamoja na tarehe mpya ya kuanza kutumika.
​​
12. Mawasiliano
Kwa maswali au maelezo zaidi kuhusu masharti haya, wasiliana nasi:
📧 vitumarkshopping (at) gmail. com
📞 +255 715 842 928